• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

WANANCHI LAJA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAEPUSHA WATOTO KUISHI 'MAGETO'....

Posted on: April 5th, 2024

Na Elinipa Lupembe

Wananchi na wakazi wa Kijiji cha Laja kata ya Ganako, wilaya ya Karatu, wamemshukuru Rais Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwajengea shule mpya ya Sekondari Laja, shule iliyowapushia gharama za kuwapangia watoto wao vyumba maarufu kama 'mageto' wakati wakienda kusoma kata za mbali.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wananchi hao wamesema kuwa, Serikali  kujenga shule katika eneo lao, shule ambayo licha ya watoto wao kupata elimu, wamekiri kuwapunguzia wazazi mzigo wa gharama za kuwapangia vyumba (mageto), miaka yote  wakiwa shuleni

"Ilikuwa mtoto akipangiwa sekondari, tulilazimika kuwapangia vyumba  karibu na shule huko Laansey, ilikuwa na gharama kubwa pamoja na usalama mdogo kwa watoto, zaidi wazazi wengi hawakuweza kumudu gharama hizo na watoto kulazimika kutembea umbali mrefu" Wamesema wananchi hao.

Wamesema kuwa, watoto wao wamepata fursa ya kusoma ndani ya eneo lao, wakati hapo awali walitembea zaidi ya Km 10 -16 kwenda na kurudi shuleni, jambo lililosababisha utoro kwa wanafunzi sambamba na baadhi kuacha shule kutokana na utoro na mimba za utotoni kwa wasichana.

Rehema Matley Amey, amesema kuwa, Serikali ya mama Samia imefanya miradi mingi katani hapo, imejenga shule ambayo imewaondolea kero na changamoto watoto ambao walitembea umbali mrefu huku kipindi cha mvua wakikosa masomo kutokana na makorongo kujaa maji lakini sasa changamoto hizo hazipo, shule imejengwa na daraja limejengwa hakuna tena watoto kukosa masomo.

"Tunaishukuru mama Samia kupitia TASAF, ilianza kwa kujenga daraja na shule ikafuata, watoto wetu waliishi kwenye nyumba za kupanga mitaani 'mageto' wakati wanasoma Kansay huku watoto  wakiishi bila usimamizi jambo ambao wasichana walifanyiwa vitendo vya ukati na wengine kuacha masomo kwa kupata mimba za utotoni" Amesema Mama Rehema

Hata hivyo, wanafunzi wa shule ya Sekondari Laja, hawakuwa nyuma, wamemshukuru Mama Samia kwa kuwajengea shule, huku wakijipongeza na kujivunia kwa kuanzisha shule mpya na kumuomba Mheshimiwa Rais kuwajengea Hosteli kwa kuwa bado wapo wanafunzi wanaotoka mbali na shule ilipo.

Emmanuel Fanueli, amesema kuwa anajivunia kwa kuwa wanafunzi wa kwanza kwa kuanzisha shule hiyo ya Laja, nakumuahidi Mama Samia kusoma kwa bidii huku akimuomba Mama Samia kuwajengea Hosteli ili wanafunzi waweze kulala shuleni.

"Tunamshukuru rais Samia ametujali watoto wa kike Laja, wengi waliacha shule kutokana na mimba za utotoni lakini  uwepo wa shule hii hapa jirani, tunamuadi Rais kusoma kwa bidii na kuwa Mwalimu" Amesema Elizabeth Mathay Niima.

Mkuu wa shule ya Sekondari Laja, Mwl. Daniel Awey Panga, amesema kuwa shule hiyo imejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 333.3 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF - OPEC IV), shule ambayo tayari wanafunzi 25 wa kidato cha kwanza, wameanza masomo mapema Januari 2024.


#ArushaFursaLukuki

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.