Idadi kubwa ya wananchi wanomiminika kupata huduma za matibabu, zinazotolewa bure kwenye Kliniki ya Madaktari Bingwa na Wabobezi Arusha, wameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Hassan na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwa huduma hiyo muhimu ambayo imetoa fursa kwa watu wasio na uwezo wa kupata huduma hizo katika mazingira ya kawaida.
Dorah Mushi ni miongoni mwa wananchi ambaye amesema kuwa, umati huo mkubwa wa watu unaashiria namna gani wanachangamoto za kiafya na wengi wao hushindwa kumudu gharama za matibabu ya kibingwa na kukiri kuwa huduma hiyo ni njema imeonyesha upendo mkubwa hasa kwa watoto na wazee.
Aidha, Bi. Dorah anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo na mapenzi yake makubwa kwa wanyonge na wazee, na kuthibitisha kuendelea kumuombea afya njema na maisha marefu zaidi, ili aendelee kuwafikia na kuwatumikia watanzania.
"Ebu angalia umati huu wa watu hata tukisema watibiwe wote haiwezekani, wengi wanasema tuongezewe muda lakini pia tuangalie na Madaktari wanatosha? Maana yake Madaktari wengine wamebaki Mahospitalini na waliopo hapa wamejitolea lakini watu ni wengi kupita kiasi.", ameongeza Bi. Dorah
Awali, kambi hiyo ya matibabu bure inafanyika kwa siku saba mkoani Arusha, ikiwa na mwitikio mkubwa wa wananchi wa Arusha na nje ya Arusha wenye changamoto za kiafya huku ndani ya siku tano ikionyesha mafanikio makubwa kwa wagonjwa ambao wamefika na kupatiwa huduma za matibabu, vipomo, dawa na vifaa tiba bure ambapo kwa wastani zaidi ya watu 3,500 wanahudumiwa kwa siku.
Kaulimbiu ya Kambi hiyo ya madaktari bingwa ni "Afya yako mtaji wako, kazi yetu ni kukupatia huduma bora"
Wizara ya Afya Tanzania Ummy Mwalimu Samia Suluhu Kwanza Ofisi ya Rais - Tamisemi Ofisi ya Makamu wa Rais CCM Tanzania
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.