• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MAONESHO YA KILIMO 88; KUJIFUNZA TEKNOLOJIA ZA KILIMO NA MIFUGO

Posted on: August 4th, 2024

Na Elinipa Lupembe 

Wananchi Kanda ya Kaskazini wamehimizwa kutumia fursa ya Maonesho ya Wakulima na Sherehe wa Nanenane, kujifunza teknolojia za kisasa kwa ajili ya kilimo, ufugaji na uvuvi na kuzitumia ili kuendeleza dhana ya Uchumi Mahalia.


Rai hiyo, imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe.Nurdin Babu wakati akifungua Maonesho hayo ya Nanenane Kanda ya Kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Nanenane Themi - Njiro, mkoani Arusha, Agosti 03,2024. 


Mhe. Babu amewasisitiza viongozi, waandaaji na watalamu wa Kilimo na Mifugo, kuwahamasisha wananchi husuasni wakulima na wafugaji kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo, ili kujifunza mbinu za kisasa za kilimo na ufugaji bora, unaoendana na mabadiliko ya kiteknolojia sambamba na mabadiliko ya tabia nchi.


"Niwaombe viongozi mlioko hapa tumieni fursa hii kuwaleta wafugaji na wakulima kutoka maeneo yenu kwa wingi ili waweze kujifunza teknolojia mbalimbali na hatimaye kuzitumia katika maeneo yao ili kuendeleza dhana ya Uchumi Mahalia (Local Economic Development)". Amesisitiza Mhe. Babu.


Aidha, amewasisitiza wananchi kuendelea kujikita na kuwekeza kwenye kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa Taifa, ambapo 90% ya wananchi kanda ya Kaskazini wakijishughulisha na Kilimo, kwa kuwa Serikali chini ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya  kilimo


Amesema kwa mwaka 2023/2024, mikoa ya Kanda hiyo, imenufaika katika utoaji wa mbolea za ruzuku, uboreshwaji wa miundombinu ya umwagiliaji na kupunguza utegemezi wa mvua katika kukuza mazao, uanzishwaji wa mashamba darasa ya malisho,uendelezaji wa viwanda vya usindikaji wa mazao ya mifugo, ujenzi wa majosho na usambazaji wa madawa ya kuogesha mifugo pamoja ugawaji wavitendea kazi kama pikipiki kwa maafisa ugani.


Hata hivyo, Mhe Babu ameagiza kufanyika tathmini baada ya maonesho hayo ili kupata picha halisi na kujibu baadhi ya maswali kadha wakadha ikiwemo kufahamu kwa undani mafunzo yapi, teknolojia ipi au zana zipi  zimekuwa na mvuto kwa wananchi waliotembelea maonesho ili ziweze kutumika kusambazwa kwa wingi katika halmashauri.


Maonesho ya 30 ya Kilimo na Sherehe za Nane Nane Kanda ya Kaskazini yanaendelea mkoani Arusha, kwenye Viwanja vya Themi  Njiro yakijumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, Kilele kikiwa tarehe 08.08.2024, yamebeba Kauli mbiu ya "Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi"


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.