Maandalizi ya Hafla fupi iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwaajili ya kuwakutanisha Wakuu wa Taasisi na Mashirika yote ya Umma nchini Tanzania na wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha. Wakuu hao wa Taasisi na Mashirika ya Umma wapo Mkoani Arusha kushiriki mkutano wa Mwaka wa Taasisi za Umma, unaoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda ambaye pia ndiye muandaaji wa Hafla hii, jana Jumatano Agosti 28, 2024 amekaririwa mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema lengo la hafla hiyo ni kubadilishana uzoefu pamoja na kutengeneza mtandao wa mawasiliano baina ya pande hizo mbili na kujadiliana masuala mbalimbali ya kiuwekezaji na kibiashara.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.