Wanariadha 5 wa timu ya Ladie's First chini ya miaka 20 kutoka Mkoani Arusha wameenda kuwakilisha mkoa kwenye mashindano ya kitaifa yatakayofanyika tarehe 23-24 Novemba, 2024 Mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza wakati akiwaaga wanamichezo hao kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Afisa Michezo Mkoa wa Arusha, Mwamvita Okeng'o amewataka kujituma kwa bidii na kuwakilisha Mkoa vizuri sambamba na kuleta ushindi Nyumbani.
kwa upande wake Kocha wa timu hiyo, Malicelina Gwandu amesema kuwa wanamichezo hao wamejiandaa vizuri kwa mazoezi ya kutosha na anatumaini kurudi na ushindi katika michezo hiyo.
Hata hivyo, Nahodha wa Timu hiyo Valeria Charles, ameahidi kwaniaba ya timu hiyo kujituma ili kupata ushindi na hatimae kufikia ndoto zao kama wanamichezo.
Michezo hiyo inahusiha mbio za za Mita 100, 200, 400, 800 na 1,500.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.