Wanawake mkoa wa Arusha washerehekea siku ya Wanawawake Duniani huku wakijivuni mabadiliko makubwa, kifkra yanaenda sambamba na mafanikio katika sekta ya uchumi na kijamii, mafanikio ambayo yamechangia kukuza pato la familia, jamii na kuchangia maendeleo ya nchi.
Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuella Kaganda, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, sherehe zilizofanyika kwenye Viwanja vya Ngarenaro, Jijini Arusha.
Amesema kuwa, kumekuwa na mabadiliko makuwa ya kwa wanawake ya kifkra, kijamii na kiuchumi, yanayotokana na uwepo wa mikakati thabiti ya uwezeshwaji wanawake, mikakati ambayo imeendelea kuleta matokeo chanya, na kuwawezesha wanawake kujikomboa kutoka katika wimbi la unyanyaswaji na ukandamizwaji, uliokuwa umetawala jamii nyingi kutokana na mila na desturi kandamizi za jamii.
Ameeleza kuwa, mafanilio hayo yametokana na jitihada kubwa, zinazofanya na Serikali ikiwa ni pamoja na kuwa Sera na mikakati jumuishi ya kumuwezesha mwanamke kujikwamua, iliyokwenda sambamba na utoaji elimu ya ujasiriamali pamoja na utoaji wa mikopo ya asilimia tatu isiyokuwa na riba.
"Serikali ya awamu ya sita, imeendelea kumsimamia mwanamke na kuhakikisha anakuwa jasiri na mwenye uwezo kwa kuitimikia jamii na taifa lake, sote tu mashahidi, utoaji wa mikopo isiyokuwa na riba imewawezesha wanawake kuanzisha biashara ndogo na kubwa na kuwafanya wanawake kujikwamua kiuchumi na kijamii" Ameweka wazi Mhe. Emmanuela.
Mhe.Emmanuela amesema kuwa, Maadhimisho haya, ya Siku ya wanawake yamekuwa ni chachu ya maendeleo na mafanikio ya wanawake, licha ya kuwaunganisha na kuwakutanisha pamoja, yamefanikisha pia kuunganisha nguvu za Asas za kijamii na ujasiri zenye kuleta ubunifu katika teknolojia jumuishi, inayoweza kufikiwa katika kupambana na ubaguzi wa kijinsia ili kuwa na jamii inayoweza kukemea na kuchukua hatua za unyanyaswaji wa wanawake na watoto wakike.
"Leo hii ni rahisi kukuta mwanamke ametoka ndani na anafanya bishara jambo ambalo hapo awali halikuwepo, tunashuhudia wanawake wa jamii ya kimaasai, wakifanya biashara huku wanaume wakiwaunga mkono, ni jambo la kujivunia sana, ni ukombozi wa kifkra na kiuchumi pia" Amesema
Aidha amewakumbusha wanawake kutambua majukumu yao ya malezi ya familia kwa kuwasisitiza kuwa, mafanikio hayo yaende sambamba na kutimiza majukumu yao kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kusimamia maadili yanayoendana na tamaduni za kitanzania pamoja na kusimamia haki za watoto kwa usawa bila kumuacha nyuma mtoto wa kiume ambaye kwa sasa yuko kwenye hatari kubwa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.