Rais Samia Hassan Suluhu ametaka wamiliki wa gereji zote nchini kuacha tabia ya kupasua magari kwenye exzosti na kutoa unga unaochochea ulevi mkubwa kwa vijana
Rais Samia aliyasema hayo jana Mkoani Arusha katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani yenye kauli mbiu isemayo Zingatia Utu,, Imarisha Huduma zaKinga na Tiba"
Alisema unga unaotoka kwenye exosti za magari unachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la madawa na kutoa rai kwa wamiliki wa gereji kubaini magari yanayopasualiwa exzosti na kutoa unga unaoleta athari kwa vijana
Alisema Tanzania imefanikiwa kuzuia uingizaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90 ambapo hivi sasa dawa za kienyeji kama bangi zimekuwa kinara katika tatizo kubwa.
Lakini pia Tanzania imepewa heshima ya kutoa mafunzo ya kemikali badhilifu katika nchi tisa na kusisitiza mkazo mkubwa uwekwe katika kupambana na madawa hayo kati ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Tanzania Bara hususan katika bandari.
Alisisitiza umuhimu wa kubadilisha taarifa za kiintelejensia na mashirika mbalimbali ya kupambana na Dawa za Kulevya ikiwemo kusimamia bandari ili Kudhibiti dawa za kulevya kuingia bandarini
Alitoa rai kwa watumishi wenye uzalendo wenye kuweka mbali maslahi ya Taifa ikiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali,na wengine wote na katika ripoti aliyoipitia ya Kupambana na Dawa za Kulevya aliona jitihada kubwa zimeelekezwa katika kutibu hususan kwa warahibu na alitoa wito kwa asasi za kiraia kutoa elimu katika taasisi mbalimbali ili vijana wajiepushe na janga hilo
Pia aliona vijana wanaopata dawa kurejea tena kuvuta madawa hayo alisema serikali inakwenda kujipanga ili kuhakikisha wanawasaidia vijana hao nakutoa rai kwa asasi za kiraia,wizara ya elimu, afya kuhakikisha vijana hao wanapata tiba ili wasirudi tena kuvuta madawa hayo.
Akizungumzia kuhusu kesi nyingi kushindwa mahakamani alisema upelekaji wa ushahidi mahamani unamapungufu alisisitiza kila taasisi zinazohusika kuwa na weledi.
Alisema muda wowote atapokea taarifa ya Tume ya Haki Jinai ili kuboresha masuala mbalimbali ikiwemo mapambano ya dawa za kulevya na kutoa rai kwa wazazi na walezi kuusimamia vema maadili ya watoto wao kuchukua nafasi zao katika kuhakikisha wanafuata njia iliyonyooka.
"Watoto wa mitaani miongoni mwao wanawazazi wao wapo sasa kati ya hao watoto wa mitaani wengi wao wanaathirika na dawa za kulevya na wimbi hili la watoto linatokana na wazazi kutowajibika"
Alitoa rai kwa wazazi kusimamia majukumu yao ikiwemo viongozi na jamii kushirikiana na viongozi wa mila ili waweze kusaidia jamii zilipo katika kusimamia maadili
Alisisitiza suala la ushirikishwaji mpana na kusisitiza kuwa familia nyingi zimeathirika hata kwa watoto wa kitajiri na kimaskini na kuongeza kuwa janga hilo ni kubwa na halichagui jinsia ila unyanyasaji wa jinsia pia upo.
"Hili nalo tukalitizame vizuri huko katika unywaji wa dawa kunaunyanyasaji wa jinsia na kichaa utamcheka sababu si wako lakini likikufika utaacha kucheka kichaa, jambo hili ni la kila mtu lazima tutengeneze jamii iliyo sawa"
Alisema serikali inampango wa kuwajengea uwezo ulio bora katika kilimo,Uvuvi,biashara pia wawe na elimu ya amali na ufundi na vyuo vya maendeleo ya jamii na pia kuwalinda kisheria.
Alisema mlinzi mkubwa wa kesho iliyobora upo kwa kijana mwenyewe hivyo nawaomba vijana mjilinde kwani serikali inawataarishia maeneo ya kupata maisha bora
Alitoa rai kwa viongozi kutumia vikundi vya sanaa ili vijana wajifunze maadili mema ili wawe viongozi bora badae.
Alisema uchunguzi unaonyesha kuwa mikoa ya Mara,Mayara, Morogoro, Iringa Ruvuma, Tanga na Kilimanjaro imeadhirika na janga hilo na kutoa rai kwa wakuu wa mikoa kuweka mikakati dhabiti ya kutoa elimu juu ya kudhibiti madawa hayo.
Aliagiza asilimia kumi ya vikundi basi asilimia nne wapate warahibu ili waweze kujikwamua kiuchumi wakiachana na dawa za Kulevya.
Kuhusu hoja ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisimiri Juu,Rais alihoji mwananchi alidhuhutu vipi kulima zao hilo bila kumwona kiongozi na hayo mavuno ya awali yalikwenda wapi kama si kwa vijana?
Alisema serikali kama ni barabara,itafika kama ni maji yatawafikia na mazao mtalima mbadala lakini naomba mlindane,viongozi onyesheni njia inashangaza kuona vijana wadogo wanaongoza magari au kubeba mzigo usiofaa sasa nashukuru kuwa mmeacha hili jani.
Alisisitiza serikali imetenga fedha sh. bilioni 24 .41 kwaajili ya kuwawezesha kupambana na kuondosha balaa hilo la dawa za kulevya.
Alisema unga unaotoka kwenye exzosti za magari unachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la madawa na kutoa rai kwa wamiliki wa gereji kubaini magari yanayopasualiwa exsozi na kutoa unga unaoleta athari kwa vijana
Awali Utafiti uliofanywa na (TMDA) maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)umebaini uwepo wa baadhi ya watumiaji wa Shisha kuchanganya dawa za kulevya aina ya heroine na cocaine na kuchangia kuwepo kwa ongezeko la biashara za dawa za kulevya.
Alitoa rai kwa jeshi la Polisi kutowabambikiza wananchi kesi kwa sababu ya chuki bali watende haki ili kuepuka chuki kwa wananchi.
Naye Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa alimkabidhi tuzo kwaajili ya kuleta maendeleo ikiwemo kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya hivyo unapaswa kupewa tuzo kama alama ya upendo na majukumu yako mazuri uliyonayo nchini.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema kwa sasa Duniani inaonyesha hakuna bangi kali zaidi kama bangi ya Arusha inayotokea eneo la Kisimiri Juu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha
Aliishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa usimamizi na uratibu wa maadhimisho hayo na mamlaka ilifika Mkoani Arusha na kwa sasa inasemekana Duniani hakuna bangi kali kama ya Arusha
"Hii inayoitwa cha Arusha naskia mpaka huko wanasema ukiingia vibaya unakuwa kichaa kwani kule inapolimwa Kisimiri juu ndio kunarutuba"
Alisema mshiri Mkuu wa kabila la Wameru, Mzee Sumary pamoja na viongozi wa dini na walitoa elimu na kuundwa kwa kamati tatu zilizoingia vijijini kwaajili ya kung'oa mimea yote ya bangi eneo la Kisimiri Juu na kazi bado inaendelea.
Naye Kamishna Jenarali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Aretas Lyimo alisema
maadhimisho hayo ni muhimu na yamekuwa yakitumika na Serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini, alimshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha sh.bilioni 2 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha warahibu kupata utaalam ili wasiweze kurudia dawa za kulevya.
Pia, ushirikishwaji wa sekta binafsi ni hatua inayostahili pongezi hususan Bandari ya Dar es Salaam itakayosaidia Udhibiti wa kemikali haribifu sanjari na dawa za kulevya.
Alimshukuru Waziri Mkuu, Majaliwa kwa kusimamia vema mamlaka hiyo pamoja na Waziri Jenista Mhagama, ambapo maadhimisho hayo yameelimisha jamii juu ya madhara na sheria inayosimamia madawa ya kulevya.
Alisema mamlaka hiyo ipo katika hatua ya kufungua ofisi ya Kupambana na madawa hayo kanda ya Kaskazini ikiwemo maandalizi ya kufungua ofisi nyanda za Kusini,Mwanza,Mbeya
Alisema, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukamata tani 7212 za madawa ya kulevya ikiwemo tani 600 zilizuiliwa kuingia nchini na kilo 20. 5 za heroine zilikamatwa na Mkoa wa Arusha bangi kavu gunia 978 zilikamatwa na bangi mbichi 465 zilikamatwa .
Tanzania imefanikiwa kupunguza uingizaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90 na Tanzania imepewa heshima kubwa ya kutoa elimu ya kudhibiti madawa katika nchi 9.
Alisema hivi sasa warahibu 14,500 wanahudumia katika kliniki zaidi ya 15 ikiwemo nyumba za warahibu yani Soba House na kuongeza Mamlaka imeungana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ili kutoa elimu mashuleni juu ya kujikinga na matumizi ya dawa za kulevya.
Alisema mikoa ya Arusha,Manyara, Morogoro ndio inayolima bangi zaidi
na kuongeza kuwa wilaya na mikoa ya Muheza,Iringa,Katavi,Manyara na mikoa mingine inahitaji kliniki za warahibu zaidi.
"Mikoa ya Tanga na Kilimanjaro ndio mikoa inayolima zaidi mirungi"
Wakati huo Waziri Jenista Mhagama alisema Rais hivi karibuni ameonyesha uvumilivu na utulivu katika utekelezaji wa dira ya maendeleo na watu walibeza hata ile filamu ya Royal Tour ambayo kwa Mkoa wa Arusha imeleeta neema na nchi kwa ujumla.
Pia, Serikali itaendelea Kupambana na uchoshaji wa kemikali haribifu zinazochochea akili kuchanganyikiwa na kusisitiza kuwa watashirikiana na vyuo vya ufundi ili kuhakikisha vijana waweze kupata ujuzi wanapotumia dawa za kulevya ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mwakilishi wa mashirika ya Kimataifa,shirika hilo linashirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha magonjwa mbalimbali yanatokomezwa ikiwemo magonjwa ya ukimwi.
Naye Ally Kayange ambaye ni Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi chini ya mfuko wa dharura wa watu wa Marekani alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anazozifanya kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchi.
Mwenyekiti kutoka Kijiji cha Kisimiri Juu,Mbayani Kuresoi alisema bangi ni zao haramu watu waache kulima na aliomba miundombinu ya barabara katika vitongoji vitatu ili kufikia wananchi kwa haraka ili biashara wanayofanya ziweze kufika kwa wakati.
Alisema wao wapo mlimani na wanahitaji miundombinu ya maji ili waweze kuwa na uwezekano wa kunyweshea mboga mboga na kuachana na zao la bangi.
Pia aliomba wawe na mazao mbadala kama mahindi,maharage,pareto badala ya kulima bangi na aliishukuru Serikali katika kaya ya Uwiro na King'ori na kuongeza kuwa uongozi wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya wameanza kuachana na dawa za Kulevya.
Alisema ameteua kamati ya watu 60 ili kuhakikisha bangi inaisha ndani ya miaka mitatu ijayo sababu bangi iking'olewa inaota tena sababu ya rutuba ya udongo.
"Kilimo cha bangi kilitufanya tukimbie polisi na watu wa Kisimiri juu hawavuti bangi ila wanauza"
Maadhimisho ya Kilele cha kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya yamefanyika Kitaifa Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ya Serikali na sekta binafsi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.