Mkurugenzi wa idara ya habari na elimu kwa mpiga kura kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi bwana Cosmas Mwaisoba, amewataka waratibu na wasimamizi wa uchaguzi kufuata maelekezo watakayopewa na tume ili wasifanye kazi kwa mazoea.
Bwana Cosmas ametoa maelekezo hayo alipokuwa akifungua mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi Daktari Charles Maela ,kwa waratibu wa mikoa,wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Amesema wanatarajia kupata uzoefu pia kutoka kwa wasimamizi wazoefu ili hata wale wasimamizi wapya waweze kujifunza mengi kutoka kwao.
Mwenyekiti wa wasimamizi wa uchaguzi Mkoa wa Arusha Daktari John Pima amesema, watahakikisha yale yote watakayo elekezwa wanayafikisha kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata huku wakifuata sheria na taratibu za uchaguzi.
Nae Mratibu wa uchaguzi Mkoa wa Arusha bwana Elgin Nkya amewashauri wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha katika maeneo yao ambayo hayafikiki kirahisi wapeleke vifaa vya uchaguzi kwa wakati ili kurahisisha upigaji kura kwa haraka.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku 3 na lengo kubwa ni kutoa maelekezo ya uchanguzi wa Rais na wabunge kwa waratibu na wasimamizi wa uchaguzi wa mikoa hiyo ya Arusha na Kilimanjaro.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.