Watu wote watakaohusika na uhujumu miundombinu ya maji kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kufungwa na faini.
Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso alipokuwa akizungumza na watumishi wa Mamlaka za Maji za Mkoa wa Arusha.
Amesema serikali imewekeza fedha nyingi sana katika miradi ya maji hivyo lazima ilindwe kwa manufaa ya wananchi wote katika Mkoa mzima wa Arusha.
Pia, amemuwagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha Eng. Justine Lujomba kuwachukulia hatua kali watumishi wote watakao waibia wananchi kwa kuwalipisha bili kubwa za maji.
Kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza wizi wa maji na utapeli unaofanywa na baadhi ya watu.
Aidha, amewataka watumushi wa mamlaka hizo kufanya kazi kwa bidii na kwa uwadilifu mkubwa ili huduma ya maji iweze kuwafikia wananchi wengi na kwa muda mfupi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta, amewataka watumishi wa Mamlaka za maji za Mkoa wa Arusha kila mmoja kutekeleza majukumu yake katika nafasi yake bila kusukumwa.
Kimanta amewataka watalaamu hao kutumia utalaamu wao kwa umakini, ili miradi ya maji inayojengwa iwe ya tija na kwa manufaa ya wananchi wa mkoa huo.
Nae, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Eng. Justine Lujomba amemuhakikishia Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Uweso kuwa mradi wa Moita katika Wilaya ya Monduli itakamilika na kukabidhiwa kwake ifikapo Aprili 19,2021.
Eng. Lujomba amewasihi watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa.
Waziri jumaa Uweso amefanya ziara ya kikazi ya siku 2 katika Mkoa wa Arusha na kukagua miradi mbalimbali ya maji iliyopo katika Mkoa huo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.