Na. Elinipa Lupembe
Wataalamu wa masuala ya Posta Afrika, wametakiwa kuendana na wakati kufuatia mabadiliko na maendeleo ya kiteknolojia katika kuwezesha sekta hiyo kufungua fursa za kiucmi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi katika nchi hizo.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Mzee Suleiman Mndewa wakati akifungua vikao vya Kamati za wataalamu wa masuala ya Posta kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), kwenye ofisi za Makao Makuu ya PAPU Mkoani Arusha, Juni 3, 2024.
Amesema kufanikiwa zaidi katika masuala ya Posta na kuendana na kasi ya ukuaji wa Biashara Mtandao, ni wajibu wao kwa pamoja kama nchi wanachama kuhakikisha kila mmoja anashiriki katika uchumi wa kidigitali kwa kutumia teknolojia za kisasa zitakazorahisisha shughuli za kiposta ili kukidhi matakwa ya wateja .
“Kupitia mkutano huu ni wajibu wetu kuhakikisha tunatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili nchi wanachama, ikiwemo miundombinu na teknolojia ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi ili kurahisisha mawasiliano kwa haraka pamoja na kukabiliana na ushindani wa soko”. Amebainisha Mhe. Dk.Mndewa.
Amebainisha kuwa ni vema nchi za Afrika kwa umoja wao kuhakikisha zinatumia teknolojia za kisiasa ili kupunguza gharama, zitakazowezesha kufikia malengo waliyojiwekea kama nchi.
Naye Katibu Mkuu wa PAPU, Dkt. Sifundo Chifu Moyo ameainisha changamoto kadhaa zinazokabili sekta ya Posta na kuwafanya wateja kutokuwa na furaha licha ya kuwa viongozi wa nchi hizo wameanza kuzitafutia ufumbuzi kwa asilimia kubwa.
Ameweka wazi kuwa, moja ya changamoto kubwa pamoja na kutikisika kwa mauzo ya Hisa katika Soko na kushuka kwa mapato, hivyo vikao vya Kamati hizo za Wataalamu vinatarajiwa kutoa majawabu ya namna Teknolojia inavyoweza kuwa suluhu, ya changamoto hizo ili kurejesha imani ya wananchi katika sekta hiyo.
Awali, mara baada ya vikao hivyo vya watamu kukamilikta vitafuatiwaa na Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la PAPU uliopangwa kufanyika kwa siku mbili Juni 11 - 12 mkoani Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.