Na Mwandishi wetu - Morogoro
Watanzania wametakiwa kuongeza uzalishaji katika sekta zote ili kukuza uchumi kwa kutumia fursa ya kuanza kutumika kwa reli ya kisasa ya kiwango cha kimataifa SGR .
Hayo yamesemwa leo Agosti 1, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliposimama katika Stesheni Kuu ya Morogoro kusalimia mamia ya wananchi waliokusanyika katika stesheni hiyo.
“Tumetumia zaidi ya trilioni 10 kujenga reli hii kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Dodoma,” alieleza Rais Dkt. Samia
Akieleza faida za mradi huo, Rais Samia amesema kuwa ni kichocheo cha maendeleo na kuwataka wawekezaji kuwekeza zaidi katika sekta zote.
Kuanza kwa shughuli za usafiri na usafirishaji kwa kutumia SGR kunapunguza muda wa safari ambapo wastani wa muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma ni masaa matatu na dakika arubaini tu.
Aidha, Rais Samia amesema kuwa reli hiyo itaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za maziwa makuu ikiwemo Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hali iyo itachochea kukua kwa shughuli za kiuchumi na kuvutia uwekezaji zaidi.
Awali Rais Samia alianza safari yake katika Stesheni Kuu ya Dar es Salaam na baadae Morogoro mbapo alisalimia wananchi katika eneo la Ngerengere na kuelekea Dodoma kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa safari za treni ya SGR.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.