Jumla ya watoto 83 wamezaliwa mkoani Arusha, usiku wa kuamkia siku ya Krismasi tarehe 25 Desemba, 2023, jambo ambalo linathibitisha ongezeko la wanawake kujifungulia kwenye vituo vya kitolea huduma za afya nchini.
Akuzungumza na mwandishi wetu , Mganga Mkuu, mkoa wa Arusha Dkt. Charles Mkombachepa, amethibitisha kuzaliwa kwa watoto hoa 83, kwenye vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri zote za mkoa wa Arusha.
Amesema kuwa, idadi hiyo ya watoto 83, watoto wa kike ni 49 na wakiume ni 34, huku wote wakiwa na afya njema na mama zao wakiendelea vizuri.
Daktari huyo amewapongeza kinamama hao, na kuwatakia malezi mema kwa watoto wao, na kuwataka kuzingatia unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa miezi 6, kuwapa kuwapeleka watoto hao kiliniki pamoja na kuhakikisha wamepata chanjo zote muhimu, huku akiwasisitiza wazazi hao kupata lishe bora.
Ikumbukwe kuwa, huu utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi - CCM, ya kuhakikisha wajawazito wanajifungulia kwenye vituo vya afya, ikiwa ni mkakati wa kutokomeza vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.