Wazazi watakao waruhusu watoto wao kufanya kazi katika mashamba ya vitunguu kukamatwa na kushitakiwa mara moja.
Ameyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo alipokuwa akizungumza na watoto na wazazi wao katika kilele cha siku ya watoto wa Afrika katika kata ya Endabash wilayani Karatu.
“Mzazi yeyote ambae ataruhusu mtoto wake akafanye kazi katika mshamba ya vitunguu,nitafanya msako na kuwakamata watoto na wao watanipeleka kwa wazazi wao na mimi nitashughulika na wazazi”.
Amesema bado tatizo ni kubwa sana hasa kipindi cha msimu wa kilimo na hivyo kupelekea watoto wengi kukosa masoma na wazazi wamewageuza kama kitega uchumi yani mtoto anatafuta analeta nyumbani kulisha wazazi badala ya mzazi atafute kulisha watoto.
Aidha, amesema bado wilaya ya Karatu inachangamoto ya uchangiaji wa chakula mashuleni kwani wazazi wengi hawataki kuchangia chakula na hivyo kusababisha watoto wengi kutofanya vizuri katika masomo yao kwasababu ya njaa.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya watoto katika wilaya ya Karatu Afisa Maendeleo ya Jamii Abdul Nyange, amesema mpaka kufika mwaka huu 2019 Wilaya ya Karatu imefanikiwa kutokomeza kabiza tatizo la watoto wa mitaa.
Amesema jitihada hizo zimefanywa na Wilaya kwa kushirikiana na taasis zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na maswala ya watoto waliopo katika wilaya hiyo, na watoto takribani 89 waliweza kupatiwa makazi ya kudumu na hivyo kupelekea tatizo hilo kumalizika kabisa katika wilaya hiyo.
Nae msoma risala kwa niaba ya watoto Christina John, amesema changamoto kubwa inayowakumba watoto katika Wilaya hiyo ni ukosefu wa elimu kwa watoto wa kike na hii inatokana na mila potofu ya kwamba mtoto wa kike hastaili kupata elimu ila ni mtoto wa kiume tu.
Pia, amesema changamoto nyingine ni wazazi kutokukubali kuchangia chakula mashuleni hii inapelekea kuwe na matabaka kati ya wanaukula na wasiokula chakula mashuleni na kudhorotesha ufauli kwa watoto.
Mimba za utoto ni changamoto nyingine inayosababisha watoto wengi kukatishwa masomo hasa wa kike kwa kurubuniwa na vijana na hata watu wazima.
Sherehe za mtoto wa Afrika ziliazishwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Afrika ya Kusini baada ya watoto wa huko kukosa haki zao za msingi na kuamua kuandama na kuzidai kwa Serikali na jamii kwa ujumla, sherehe hizi zimekuwa zikiazimishwa kila mwaka mwezi Juni na mwaka huu 2019 Kimkoa yamefanyika Wilayani Karatu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.