Walengwa 7,652 wamenufaika na mradi wa ACHIEVE katika maswala mbalimbali ikiwemo kuwashonea sale za shule watoto 430, kujiunga na elimu ya ufundi VETA na kuwanunulia vifaa watoto 6, kutoa chakula na lishe bora kwa watoto 4,279, kutoa ulinzi na usalama kwa watoto na vijana 1,467, utoaji wa elimu ya malezi na makunzi kwa walezi 1,650 na kuwanufaisha kiuchumi walezi 2,208 katika halmashauri ya Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha.
Taarifa hiyo imetolewa na afisa Afya Mkoa Vones Uwisso kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia katika kikao cha makabidhiano ya mradi wa ACHIEVE kutoka shirika la Pact Tanzania kwenda kwa mradi wa Kizazi hodari chini ya shirika la ELCT.
Amelikata shirika hilo kuhakikisha mradi huo unafika katika halmashauri vyingine kama vile Ngorongoro, Karatu, Monduli, Longido na Meru ili ziweze kunufaika pia na mradi huo na kuokoa maisha ya watoto wengi katika Mkoa wa Arusha.
Mradi wa ACHIEVE ulilenga kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika jamii ya Mkoa wa Arusha na juhudi hizo zitaendelezwa na mradi huo wa Kizazi Hodari.
Mradi wa ACHIEVE ulinza Agosti 2021 na utamalizika Juni 2022 katika halmashauri mbili za Arusha Jiji na Arusha katika Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.