Watu wa tatu wamefariki Dunia baada ya kufukiwa na Kifusi wakati wakiwa wanapakia Molamu katika machimbo ya Kisongo, Kijiji cha Engolola na wengine watatu wakiwa ni Majeruhi.
Dereva wa Lori lililokuwa linapakia Molamu hiyo bwana Iddi Rashidi anasema jumla ya watu waliokuwa eneo la tukio ni sita na watatu kati yao wamefariki Dunia na watatu wamejuruhiwa na wameshapatiwa matibabu katika Zahanati ya Kisongo.
Akitoa salama za pole kwa familia na wachimbaji, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta amewataka wachimbaji hao kuchukua tahadhari pindi wanapofanya shughuli zao kutafuta riski katika maeneo hayo kwani siyo salama sana.
Aidha, Kimanta amesema serikali inachukua hatua za haraka za kuwapeleka wataalamu wa Madini katika Machimbo hayo ili wakafanye uchambuzi wa kina na kupendekeza njia zipi zitafaa kutumika katika uchimbaji wa Molamu na kwa usalama zaidi.
Pia, amewataka wataalamu hao wa Madini kuhakikisha wanatembelea Machimbo yote ya Molamu yaliyopo katika Mkoa wa Arusha na kutoa elimu ya uchumbaji bora na salama kwa wachimbaji wa Molamu.
RC Kimanta amewataka wachimbaji hao kuunga Mkono mapendekezo yatakayotolewa na wataalamu hao na kuyafanyia kazi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.