KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA AFANYA ZIARA MOUNT MERU
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Mhe. Missaile Abano Musa amefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kuongea na watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru leo Agosti 24, 2022, ikiwa ni moja ya ziara za mwanzo kati ya alizozifanya tangu ateuliwe kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha.
Akitembelea Miradi hiyo ya maendeleo ambayo imegharamikiwa kwa fedha za serikali ikiwa kwenye hatua za mwisho kumalizika na kuanza kutumika, Katibu Tawala ameupongeza Uongozi wa Hospitali kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo na kutekelezwa ndani ya muda uliowekwa ili kuwezesha kuongezeka kwa huduma bora zinazotolewa hospitalini.
Vilevile, aliweza kupata wasaa wa kuzungumza na watumishi wa hospitali na kusisitiza wafanye kazi kwa weledi katika kutimiza majukumu yao ya kufikisha huduma bora za Afya kwa jamii na kuwahaidi ushirikiano baina ya Ofisi yake na hospitali katika kutimiza majukumu hayo.
Miradi hiyo ya maendeleo iliogharimu jumla fedha taslim Tsh. Billioni 4.444 ni pamoja na upanuzi wa jengo la dharura (EMD), ukarabati ya wodi ya wagonjwa mahututi (ICU), ukarabati wa wodi ya watoto, ukarabati wa jengo la mazoezi na matibabu kwa njia ya matandao, ununuzi wa mashine ya kisasa ya mionzi (Digital Xray), ununuzi wa mashine ya CT Scan na ujenzi wa nyumba ya mtumishi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.