Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha, wakimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, ya kumpongeza na kumshukuru kwa uongozi wake imara, unaowawezesha, watumishi hao kufanya kazi kwa amani, upendo na ushirikiano unawapa fursa ya kuwajibika na kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi kwa wepesi zaidi.
Aidha, watumishi hao, licha ya kumkabidhi zawadi hiyo ndogo, kama ishara ya upendo, zaidi wamemuombea baraka nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja na kumtakia maisha marefu yenye afya njema.
Watumishi hao, wempongeza Kiongozi huyo, wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2024, iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha, ukumbi wa Nyasa, Jijini Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.