Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha watumishi wote wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu wanapata stahiki zao kwa wakati.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi pamoja na wananchi katika ziara yake wilayani humo katikati ya juma hili.
Amesema nimejionea watumishi wanavyofanya kazi kwenye Hospitali ya wilaya ya Malinyi, wanafanya kazi kwa moyo, wanajitoa kuwahudumia watanzania sasa watumishi kama hawa na wale walioko kwenye maeneo mengine ya namna hii wasîkatishwe tamaa kwa kucheleweshewa stahili zao wapewe kwa wakati’
Sitaki kusikia mtumishi hajapanda daraja,sijui hajapewa fedha za likizo na marupurupu mengine nataka kuona watumishi wa pembezoni wote wanapanda madaraja kwa wakati na hili ni kwa Wakurugenzi wote nchini’ Amesisitiza
Na Nyie watumishi niendelee kuwatia moyo kuwa kazi mnayofanya ya kuwahudumia watanzania ni ya muhimu sana kwa Taifa letu mnahakikisha maono ya Rais Dkt. Samia yanatimia kwa wananchi hawa wa pembezoni kupata huduma bora kama wale wa mjini niwahakilishie hapa mnapata thawabu kwa Mungu aliongeza.
Sitapenda kuona mtumishi anayefanya kazi kwenye mazingira mahumi anasononeka au kuumia kwa kukosa stahiki zake kila Mkurugenzi ahakikishe watumishi wa maeneo kama hayo wanapata haki zao kwa wakati ili waweze kufanya kazi zao kwa amani’ alisisitiza Mchengerwa!
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.