Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema jumla ya shilingi bilioni 243 zimeshatengwa kwa ajili ya kupandisha madaraja watumishi wote.
Amesema hayo alipokuwa akifungua mkutano Mkuu wa 8 wa Makatibu Mahususi uliofanyika Jijini Arusha.
Serikali itawapa shahiki zao zote ikiwemo ya kuwapandisha madaraja Makatibu Mahususi hao.
" Serikali haijawasahau katika kuwapandisha madaraja, kwani ni haki yenu ya Msingi katika utumishi wa Umma".
Mchengerwa amesema kumpandisha daraja Mtumishi ni kumuongezea hali ya kufanya kazi kwa uwaminifu na weredi mkubwa zaidi kuliko kutoka mpandisha kwani kunamkatisha tamaa ya kufanya kazi.
Aidha, Mhe.Mchengerwa amewataka Makatibu Mahususi hao kuhakikisha wanabadilika kwa kufanya kazi kwa uwaminifu mkubwa hasa kutunza siri za ofisi zao.
Mwenyekiti wa chama cha makatibu Mahususi (TAPSEA) Bi. Zuhura Maganga amesema, waajiri wao wanatakiwa kuitambua fani hiyo na kuitumia ipasavyo katika kuongeza ufanisi wa kazi katika maofisi yao.
Amesema changamoto kubwa inayoikabili tasnia hiyo ni kutopata nafasi ya kuhuzuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi ili kujijengea uwezo wa kumudi majukumu yao zaidi.
Pia, wameomba wabadilishiwe muundo wa utumishi katika tasnia hiyo kwani kwa sasa kuna ngazi ya shahada na bado haijaweza kutambulika vizuri katika muundo huo .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amesema, kada ya Makatibu Mahususi ni ya muhimu sana katika utendaji wa kazi za ofisi, hivyo inatakiwa iheshimiwe na kuthaminiwa sana.
Amesema ofisi bila Makatibu Mahususi kazi nyingi zitachukuwa muda mrefu kukamilika au nyingine kutokamilika kabisa.
Zaidi ya Makatibu Mahususi zaidi ya 3000 waliweza kuhuzuliwa mkutano huo iliokuwa na lengo la kuwajengea uwezo zaidi katika utendaji wa kazi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.