• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

WAZIRI GWAJIMA AHIMIZA JITIHADA ZAIDI, UKOMBOZI WA WANAWAKE DHIDI YA UKATILI.

Posted on: February 25th, 2025

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Dkt. Doroth Gwajima ameupongeza Mkoa wa Arusha kwa maandalizi mazuri kuelekea wiki ya wanawake duniani, akihimiza jitihada zaidi kwenye utekelezaji wa mikakati ya kuwainua wanawake katika nyanja mbalimbali pamoja na kuondoa unyanyasaji na ukatili wa aina mbalimbali kwa wanawake na wasichana.



Wakati akizungumza na wajumbe wa kamati mbalimbali za maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya mwanamke duniani Machi 08, 2025, Waziri Dkt. Doroth Gwajima amesisitiza pia umuhimu wa Mkoa wa Arusha na mikoa mingine kote nchini, kuendelea kutoa elimu ya afya, Mikopo kwa wanawake sambamba na kuwafahamisha wananchi kuhusu fursa za uwezeshaji wanawake kiuchumi.



Akikemea udhalilishaji na ukatili wa kijinsia unaotokana na baadhi ya tamaduni katika Mikoa ya Arusha na Manyara inayopelekea ukeketaji kwa wasichana, Dkt. Gwajima amesisitiza umuhimu wa kubuniwa mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili huo ili kubadilisha sura na takwimu za unyanyasaji katika Mikoa hiyo pamoja na kutokomeza fikra na tamaduni za kale zisizokuwa na faida kwa zama hizi.



Katika mazungumzo yao, Mhe. Makonda ameeleza kuwa Mkoa wa Arusha upo tayari kwaajili ya Siku ya mwanamke duniani ambapo maadhimisho yake Kitaifa yanatarajiwa kuwa Machi 08, 2025 Jijini Arusha na Kuongozwa na mgeni rasmi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema katika Juma la kuelekea Machi nane, shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo elimu mbalimbali na utoaji wa elimu na msaada wa kisheria kwa wasichana na wanawake wa Mkoa wa Arusha pamoja na mashindano ya michezo ya aina mbalimbali kwaajili ya wanawake  kando ya burudani nyingine zitakazotolewa na wanawake ikiwemo mbio za magari na muziki kutoka kwa wanawake wanaounda bendi mbalimbali.



Kikao hicho pia kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, kilihudhuriwa na washauri wa Rais Mhe. Angellah Kairuki pamoja na Mhe. Sophia Mjema, Katibu tawala Mkoa wa Arusha Musa Missaile, wadau mbalimbali kutoka Taasisi za kifedha na wa masuala ya wanawake pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi CCM na serikali.


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.