Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameagiza kukamilika kwa ujenzi wa bwalo la chakula shule ya sekondari ya Longido Samia Girls ifikapo Novemba 01, 2024, ujenzi ambao umefikia kwenye boma.
Mhe. Mchengerwa ametoa agizo hilo alipotembelea shuleni hapo kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa shule hiyo mpya ya mkoa wa Arusha, ambayo tayari wananfunzi wa kidato cha tano wameanza masomo shuleni hapo.
Amemtaka mkuu wa wilaya ya Longido Mhe. Salum Kali kusimamia kwa karibu na kuhakikisha mafundi wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa bwalo hilo la chakula na wananfunzi waanze kulitumia kama yalivyo makusudio ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hasan.
Wakandarasi wananojenga bwalo hili
Hata hivyo amewahimiza kukamilika kwa bwalo hilo, kuendana na matumizi ya nishati safi katika kupika chakula cha wananfunzi na kuachana na kuachana nishati chafu yenye madhara kwa bianadamu.
"Tunatakiwa kuzingatia matumizi ya nishati safi kwenye shule zote za sekondari ili kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais, katika kuhamasisha matumizi ya Nishati safi nchini" Amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Awali mradi wa ujenzi wa shule mpya ya wasichana Longido Samia Girls umetekelezwa na Serikali kwa kutoa fedha kwa awamu mbili awamu ya kwanza ikitoa milioni 300 na awamu ya pili milioni 1.45 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bwalo la kulia chakula.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.