Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ameahidi kuomba fedha kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwaajili ya kuongeza nguvu za Ujenzi wa madarasa nane kwenye shule ya Sekondari Kiutu, Halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Mhe. Mchengerwa ametoa ahadi hiyo mapema leo Oktoba 02, 2024, alipotembelea shuleni hapo kwa lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Kiutu, iliyojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 800 kupitia programu ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari nchini (SEQUIP) na kuahidi kuongeza fedha za kujenga vyumba 8 vya madarasa shuleni hapo.
Mhe. Mchengerwa amefurahishwa na hali ya maendeleo ya shule hiyo yenye jengo la ghorofa tatu ikiwa na takribani wanafunzi 500, na kumuagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI na Mkurugenzi wa Elimu kufika kwenye Shule hapo na kufanya tathmini ili kufahamu gharama za ujenzi wa madarasa hayo nane ambayo wizara ya TAMISEMI itayajenga.
Hata hivyo Mhe. Mchengerwa amewapongeza wananchi, uongozi wa wilaya na halmashauri na mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Chritiana Makonda, kwa kuwaunganisha wananchi na kuwafanya kujitolea na kuchangia shughuli za Maendeleo, kwa manufaa ya Umaa huku akitoa pongezi nyingi kwa Diwani wa kata ya Kiutu Mhe. Malaki Malambo kwa kutoa eneonlake la Mita za mraba 6,400 na kujenga shule hiyo ya Kiutu.
"Ninawaponheza wananchi wote, watalamu, mkurugenzi, Mbunge Baraza la Madiwani kwa ushirikiano wenu kwa manufaa ya Umma, nikupongeze Mheshimiwa Diwani kwa kjitoa kwa ajili ya wananchi wako, niwaombe Madiwani wote nchini kuiga mfano huu wa kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya wananchi waliowachagua" Amesema
Awali Mhe. Mchengerwa yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ikiwa ni awamu yake ya pili ya ziara Mkoani hapo yenye lengo la kukagua hali ya utekelezaji wa shughuli wa maendeleo ikiwemo mirafi pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.