WAZIRI MCHENGERWA ATAKA WENYE SIFA KUJITOKEZA KWA WINGI KUWANIA NAFASI MBALIMBALI SERIKALI ZA MITAA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe.Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi wote wenye Sifa kujiandaa na kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kwenye serikali za mitaa pale dirisha hilo litakapofunguliwa Oktoba 26 mpaka Novemba Mosi ya Mwaka huu 2024.
Mhe. @mohamed_mchengerwa amebainisha hayo mapema leo Jumapili Oktoba 20, 2024 alipokuwa akitoa tathimini ya zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la mpigakura,na kuwapongeza wananchi wote waliojiandikisha kwakuwa wametumia haki yao ya Kikatiba ya kutekeleza baadhi ya kanuni ili kuweza kuwachagua Viongozi wawatakao kwa maendeleo ya Vijiji,Mitaa na Vitongoji vyao.
Awali Mhe. Mchengerwa naye alijiandikisha kwenye daftari la Mpigakura kwenye eneo la Mchikichini na kutoa wito kwa wasimamizi wa Uchaguzi na wadau wake wote kuhakikisha kuwa sheria, taratibu na miongozo mbalimbali inafuatwa ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, haki na wenye kuzingatia falsafa ya 4R ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.