Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB),ametembelea banda la Vikundi vya Wanawake wajasiriamlia Jiji la Arusha, kwenye Maonesho ya 3 ya Wiki ya Huduma za Kifedha, yanayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Vikundi vya Wanawake wajasiriamali Jiji la Arusha, Bi. Husna Almas, amepata fursa ya kumuelezea Waziri Mkuu, shughuli mbalimbali, wanazozifanya wajasiriamali hao, pamoja na kuwasilisha ombi lao kwa serikali
Kwa niaba ya vikundi vya wanawake wa mkoa wa Arusha, Mwenyekiti Husna, ameiomba Serikali yao ya awamu ya sita, kurejesha Mikopo isiyokuwa na riba, iliyokuwa onatolewa na Serikali, kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri zao, kwa kuthibitisha kuwa, mikopo hiyo iliwainua wanawake kwa kukuza mitaji na kuongeza pato la familia na taifa.
Hata hivyo Mheshimiwa Waziri Mkuu, ameigaiza Ofisi ya Rais - TAMISEMI, kuharakisha ukamilishaji wa mchakato ulioelekezwa na Serikali, wa namna bora ya utoaji wa mikopo ya isiyokuwa na riba, ili ifikapo Januari 2024, vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waanze kupata mikopo na kunufaika na fedha hizo za serikali yao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.