Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa Felician Mtahengerwa , kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, asubuhi ya leo Agosti 20, 2024.
Mhe. Majaliwa amefika mkoani Arusha kwa ndege ya shirika la ndege Tanzania (ATC) tayari kwa kufungua Kongamano la tatu la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST), linalofanyika kwenye kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha - AICC, ukumbi wa Simba Jijini Arusha.
Kongamano hilo la siku 5 lililowakutanisha madereva wa Serikali nchini, limeanza tarehe 19 - 23 Agosti, 2024, lililobeba Kauli Mbiu ya "Dereva wa Serikali Jitambue,Timiza Wajibu wako, Usalama Barabarani Unaanza na wewe".
Ofisi ya Waziri Mkuu Ofisi ya Rais - Tamisemi Wizara Ya Uchukuzi Ikulu Mawasiliano Samia Suluhu Kwanza
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.