Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameondoka mkoani Arusha Leo na kusindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania, leo Februari 18, 2024
Waziri Mkuu ameondoka mkoani Arusha baada ya kukamilisha shughuli z amsiba na hatimaye mazoshi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa, yaliyofanyika kijij8 cha Ngarashi wilaya ya Monduli Februari 17, 2024
Hata hivyo, Mhe. Mongella amemshukuru Waziri Mkuu, watalamu na timu nzima kutoka ofisi ya Waziri yake kwa kujitoa kufanikisha shughuli za mazishi ya Hayati Lowassa na kuongeza kuwa haikuwa kazi nyepesi ili kutokana na ushirikiano mkubwa mkubwa mkoa ulioupata kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, shughuli zilikwenda vizuri na kukamilika bila mikwamo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.