Waziri Mkuu wa Rwanda, Mhe Ngirente Edward, amewasili nchini Tanzania jioni ya leo na kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Balozi Fatou Hererimana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella, kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA), kwa ndege ya Shirika la ndege Rwanda ( Rwanda Air)
Waziri Mkuu huyo, amewasili nchini, kwa ajili ya kushiriki, Mkutano Mkuu wa Mwaka, unaohusisha Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki ( 23rd Ordinary Summit of East Africa Community Head of States), unaotegemea kufanyika Mkoani Arusha, tarehe 23-24 Novemba, 2023, kwenye Hoteli ya Ngordoto Mountain Lorge, wilayani Arumeru.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.