Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Machi 06, 2025 amekutana na kuzungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS Wakili Boniface Mwabukusi ambapo pamoja na mengineyo, wamekubaliana kushirikiana katika kusikiliza na kutatua kero za ardhi zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Mhe. Makonda amenukuliwa mara kadhaa akisema kuwa Arusha ni miongoni mwa Mikoa yenye migogoro mingi ya ardhi na Kufika kwa Mhe. Ndejembi ambaye ataungana na Wakili Mwabukusi na wanasheria wanaohudumu kwenye kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia, kunatokana na ombi la Mhe. Makonda alilolitoa kwa Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, akiomba usaidizi wa Wizara hiyo katika utatuzi wa migogoro mikubwa ya ardhi ambayo imekuwepo Mkoani hapa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.