Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Damian Ndumbaro, amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya CRCEG, iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa Uwanja wa mpira wa miguu Arusha, kuhakikiza mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyoainishwa kwenye mkataba.
Mhe. Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo, wakati wa hafla ya Kumkabidhi Mkandarasi eneo la ujenzi wa uwanja huo, iliyofanyika kata ya Olmoti, Jijini Arusha.
Amesema kuwa, Serikali inayomalengo na maelekezo kutoka FIFA ya kutumia uwanja huo kwenye mashindano ya AFCON mwaka 2027 na mkataba wa mradi huo ni miezi 24, na kumsisitiza mkandarasi kuzingatia mkataba lakini zaidi viwango vya ubora.
Aidha, ameuagiza uongozi wa mkoa wa Arusha, kupitia Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kushughulikia vibali vyote muhimu vya ujenzi, ili mkandarasi huyo asikwame kufanya kazi yoyote.
"Mkandarasi huyu apewe ushirikiano na asikwamishwe kwa namna yoyote ile, ni jukumu lako Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, kuhakikisha anapata vibali vyote vinavyohitajikankwenye ujenzi, asitokee mtu wa mazingira au afya kumuuliza mkandarasi vibali, wekeni mazingira rafiki ya kumpatia vibali vyote".Amesema Dkt. Ndumbaro
Aidha, ameuelezea mkakati wa Serikali ya awamu ya sita kuamua kujenga uwanja huo Arusha licha ya mashindano ya AFCON ni fursa ya kiuchumi kwa mkoa wa Arusha, inayokwenda kuchagiza utalii wa asili na kupanua wigo katika utalii wa michezo, utakao ongeza pato na uchumi wa Taifa.
"ipo mikoa mingi yenye maeneo makubwa, iliyoomba na kutamani uwanja huu ujengwe huko, lakini kura ikaangukia Arusha, ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kukuza sekta ya utalii ikiwemo utalii wa michezo, kupitia uwanja huu wageni wote wapenda soka na watu maarufu dunia watakuja kwenye michezo jijini Arusha" Amesisitiza Dkt. Ndumbaro
Hata hivyo, amewataka wananchi wa Arusha, kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapa fursa hiyo adhimu ya ujenzi wa uwanja inayokwenda kuleta mabadiliko chanya ya kuchumi Arusha na kuwataka kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi pamoja na kushirikia katika kazi zitakazohitaji utalamu wa ndani.
Awali,Serikali kupitia Wizara yenye dhamana, imemkabidhi Mkandarasi eneo lamujenzi waUwanja wa mpira wa miguu Arusha, rmradi utakaotekelezwa kwa miezi 24.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.