Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Jerry Silaa (MB), amewaagiza Wakurugenzi wa Wizara hiyo, kuweka kambi Jijini Arusha kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kushughulikia masuala yote yanayohusu ardhi ikiwemo kuandaa mipango miji, kufanya tathmini na kutoa hati miliki za maeneo yote yanayozunguka eneo linalojengwa uwanja wa mpira wa Miguu Arusha.
Mhe. Silaa amatoa agizo hilo, alipokuwa akizungumza na wananchi, kwenye hafla ya kumkabidhi Mkandarasi eneo la kujenga uwanja huo wa mpira, hafla iliyofanyika kata ya Olmoti, jijini Arusha na kuwataka Wakurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka wizara ya Ardhi, kuweka kambi Jijini Arusha ili kuhakikisha wanakamilisha kazi zote zinazohusu masuala ya ardhi ndani ya siku 90 hati zote ziwe zimepatikana.
Amesema kuwa, tayari Mkandarasi ameshakabidhiwa eneo la ujenzi wa uwanja ambao mkataba wake unakamilika na kukabidhi uwanja mapema mwaka 2026, huku akisistiza kuwa, ucheleweshwaji wa aina yoyote ile, utakaosababishwa na Wizara yake hatauvumilia.
"Leo hii Serikali kupitia Wizara yenye dhamana na Michezo, imemkabidhi Mkandarasi 'site', bado kuna maeneo yanatakiwa kulipwa fidia na yapo yanayotakiwa kupimwa na kutolewa hati miliki, ili mazoezi yote yaende sambamba na ujenzi wa uwanja, ni lazima watalamu wa Ardhi watoke ofisini wahamie hapa Olmoti, watalamu wa Wizara washirikiane na watalamu wa Jiji la Arusha, ili ndani ya sku 90 kazi zote zinazohusu ardhi zikamilike" Ameagiza Mhe. Silaa
Aidha, ameongeza kuwa, Serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa sana katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, kazi ya watalamu ni kuwajibika kila mmoja kwa nafasi a taaluma yake na kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa bila kuwa na kikwazo na kuongeza kuwa, mtalamu atakayeshindwa kwenda na kazi na kutimiza wajibu wake, utakaokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo hatavumilika badala yake, mtalamu huyo atalazimika kukaa kando.
Awali, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Damian Ndumbaro amemkabidhi Mkandarasi wa eneo lamujenzi wa uwanja, Mkandarasi wa Kampuni ya CRCEG ya nchini China kwa gharama ya shilingi Bilioni 286, mradi unaotegemea kukamilika mwaka 2026.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.