Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, amewataka wajasiriamali kote nchini kuhakikisha wanaweka mananeo ya kuitangaza nchi katika bidhaa zao.
Ametoa maagizo hayo alipokuwa akifungua maonesho ya 4 ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi Kanda ya Kaskazini, yaliyojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga.
Amesema ili nchi yetu na bidhaa zetu ziweze kutambulika zinatakiwa kutangazwa hasa kwa kuweka maneno kama vile (Made in Tanzania), ili kupata masoko na kuitangaza nchi ndani na nje.
“Ni aibu sana tuna bidhaa nzuri na bora lakini hazijulikaniki kama zinatoka katika nchi yetu”,alisema
Aidha, amelitaka baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi kuhakikisha elimu inawafikia wananchi juu ya namna mifuko hiyo inavyofanya kazi hususani kwenye masharti ya mikopo.
Mifuko mingi haijulikaniki kwa wananchi, hivyo kupitia maonesho haya elimu isambawe kwa watu ili watu waifahamu mifuko hiyo na kuwawezesha kupata mikopo kwa wigi.
Mwenyekiti wa baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi Festus Limbu amesema ili wananchi wengi waweze kunufaika na mifuko hiyo ni vizuri ukawezeshwa ili kuwa na wigo mpana wa kuwawezesha wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Mikirikiti amesema,wenye jukumu la kuwasimamia na kuwaongoza wajasilimali ni viongozi hao wa Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chini.
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta amesema, maonesho hayo yatatumika kama madarasa ya kutoa elimunya mfuko kwa wananchi ili fursa za uwekezaji ziweze kukua katika kanda ya Kaskazini.
Kimanta amesema, wananchi wengi wanachangamoto ya mitaji katika kuanzisha au kukuza biashara zao lakini wengi hawana uwelewa wa namna ya upatikanaji wa mikopo kutoka katika mifuko hiyo.
Hivyo, ameitaka mifuko hiyo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kuhakikisha wanatoa ushirikiano mzuri hasa katika kutoa maelezo yaliyojitosheleza kwa wananchi ili waweze kujifunza na kuielewa mifuko hiyo.
Jumla ya mifuko 54 ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ipo Tanzania na mifuko 20 inawawezesha wananchi moja kwa moja na kiasi cha shilingi trilioni 2.2 zimetolewa kama mikopo kwa watu milioni 4.9 huku taasis 5000 zimeshanufaika kwa miaka mitano iliyopita 2015 hadi 2020.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.