Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amesema ofisi yake itaanzisha dawati maalumu kwa ajili ya kusimamia maswala ya uwekezaji katika Mkoa wa Arusha.
Ameyasema hayo alipofanya kikao kazi cha kusiliza changamoto zilizopo katika sekta ya kilimo cha Mbogamboga, Matunda na Mauwa kutoka kwa wadau wa sekta hiyo.
Aidha, amewaomba wawekezaji waliopo katika Mkoa wa Arusha kuwa mabalozi wa kuisemea vizuri nchi ya Tanzania na hata Mkoa wa Arusha ili kuwavutia wawekezaji wengi kutoka nje.
Mongella amesisitiza kuwa katika uongozi wake ameweka vipaombele katika sekta ya Elimu, Viwanda, uwekezaji na Kilimo ili kukuza uchumi wa Mkoa.
Pia amewashauri wafabiashara wa bidhaa mbalimbali kufunga bidhaa zao kwenye vifungashio vinavyovutia na vyenye nembo ya kuitambulisha nchi ya Tanzania.
Amesisitiza kuwa uwekaji wa nembo hiyo kutaitangaza nchi ya Tanzania ndani na nje na kukuza masoko ya kwa wafanyabiashara hao.
Nae, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya TAHA Jacqueline Mkindi amesema, sekta hiyo bado inakabiliwa changamoto nyingi ikiwemo vikwazo vingi katika usafirishaji wa bidhaa hizo.
Gharama kubwa katika uzalishaji, pia kuna uhaba wa wasafirishaji wa bidhaa hizo na uchache wa masoko.
Aidha, ameiyomba Serikali kuunda kamati maalumu ya kusimamia sekta hiyo itakayojumuisha taasisi binafsi na Serikali na pia kusamehe madeni kwa baadhi ya mashamba yanayodaiwa ili kuwaruhusu wawekezaji wengine waweze kuwekeza katika Mashamba hayo.
RC Mongella amesema kikao hicho na sekta ya Mbogamboga, Matunda na Mauwa ni mwanzo tu, kwani atakutana na sekta zote za kipaombele ili kufahamu changamoto zao na kuweka mazingira ya kufanya kazi kwa pamoja.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.