Shirika la Chakula Duniani (WFP) limekuja na mpango wa kukabiliana na majanga ya ukame na mafuriko kabla hayajaotokea, mradi ambao wanatarajia kuutekeleza kwenye wilaya za Longido na Monduli Mkoa wa Arusha.
Akizungumza mara baada na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, ofisini kwake leo, Mratibu Programu ya kupambana na majanga kutoka WFP, Dkt. Elisha Moyo, amesema kuwa, wamefika mkoani Arusha, kwa lengo la kutambulisha mradi wa kukabiliana namajanga ya ukame na Mafuriko mradi ambao, unatarajiwa kuzinduliwa katika wilaya hizo mbili, mwanzoni mwa mwezi Februari 2024
"Programu hii tofauti na nyingine, inategemea kuelimisha jamii kujiandaa kukabiliana na majanga ya ukame na mafuriko kabla hayajatokea, zimechaguliwa wilaya hizo kutokana na changamoto hizo kutokea mara kwa mara, katika maeneo ya wilaya hizo"
Naye Katibu Tawala Mkoa, amewashukuru na kuwakatibisha mkoani humo, kwa ajili ya kuendesha program hiyo ambayo ni muhimu kwa wananchi wa maeneo hayo, kutokana na madhara yanayowakumba wananchi pindi yanapotokea mafuriko na ukame.
Aidha, amewaahidi kutoa ushirikiano kupitia watalam wa ngazi zote, kuanzia ngazi ya mkoa mpaka kijiji ili kuhakikisha kuna kuwa na jamii salama isiyo na majanga kama ukame na mafuriko.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.