Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 umepitia jumla ya miradi 9 katika Wilaya ya Ngorongoro nakuridhishwa na miradi yote.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bwana Abdalla Kaim ameipongeza Wilaya ya Ngorongoro kwa kupata hati safi katika miradi yote iliyopitiwa na Mwenge Uhuru na kuwataka watekeleze maagizo yote yaliyotolewa na Mwenge huo kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.
Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi 9 ikiwemo ya Mazingira, afya, Miundombinu, shule, mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi,klabu ya rushwa iliyogharimu zaidi ya sh.bilion 1.
Katika miradi hiyo,mradi 1 uliwekewa jiwe la msingi,miradi 2 ulifunguliwa, mradi 3 ulizinduliwa na miradi 3 ilitembelea.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekimbizwa katika Wilaya ya Ngorongoro kwa umbali wa kilomita 305.57 na zimemaliza kwa Mkoa mzima wa Arusha. Mwenge wa Uhuru unatarajia kukabidhiwa katika Mkoa wa Mara Julai 4,2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.