*Aliyosema Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka*
#Serikali itayachukua maazimio yote na nawaahidi yatafanyiwa kazi na tutawasaidia kuhakikisha yanatekelezeka kwa sababu ndoto ya Mhe. Rais ni kuhakikisha tunakuwa na mashirika yenye ufanisi mkubwa wa viwango vya kimataifa na uwezo mkubwa wa kuchangia katika Pato la Taifa.
#Nawakumbusha ulazima wa kutekeleza maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais Samia, ni lazima yatekelezwe kwa ukamilifu wake.
#Jitihada kubwa zinahitajika kuendelea kuimarisha usimamizi wa taasisi za umma ili kuongeza ufanisi na tija kwani serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa taasisi hizo hivyo, inategemea kupata manufaa.
#Nasisitiza kuwa, ni wajibu wa kila taasisi kuandaa na kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kitaasisi wa kupambana na rushwa, ni muhimu kuimarisha mifumo ya usimamizi.
#Ni lazima kuzingatia sheria kwenye uandaaji wa mikataba, uingiaji na usimamizi wake. Aidha, nawakumbusha kutimiza wajibu wenu katika kutekeleza maazimio ya mwaka 2024 na yale ambayo hayakukamilika mwaka 2023
#Nawataka kuimarisha mifumo ya mawasiliano ndani ya taasisi na baina ya taasisi ili kuongeza ufanisi na kuweza kwenda kwa pamoja.
#Namtaka Msajili wa Hazina atekeleze kikamilifu mfumo wa kupima ufanisi wa taasisi na mashirika ya umma ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali.
#Viongozi wa taasisi na mashirika ya umma wajenge utamaduni wa kujifunza mbinu na mikakati mipya kutoka kwa mashirika yaliofanikiwa, tujifunze kutazama serikali kwa upana wake.
#Mhakikishe mnaweka mifumo mizuri ya usimamizi ili kuhakikisha watumishi walio chini yenu wanafanya kazi
#Mnatakiwa kuhakikisha mifumo ya TEHAMA inasomana, tunafanya hili kwa sababu ya kuongeza ufanisi katika kazi. Tayari Mhe. Rais Samia ametoa muda wa kukamilisha hadi mwezi Disemba, 2024.
#Natoa agizo ndani ya mwezi huu wa Septemba, viongozi wa taasisi na mashirika ya umma kuhakikisha wameshirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao kuondoa changamoto zilizopo kabla ya mwezi Disemba kufika.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.