Na.Edmund Salaho/ Dar es Salaam
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikiana na makampuni ya waongoza watalii nchini imepanga kuwapeleka watanzania zaidi ya 500 katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kusherehekea siku ya uhuru kupitia kampeni ya “Twenzetu Kileleni 2024” ikiwa ni msimu wa Nne wa Kampeni hiyo yenye Kaulimbiu isemayo “Stawisha Uoto wa Asili Tanzania, Okoa Barafu ya Mlima Kilimanjaro” kampeni ambayo imezunduliwa leo Septemba 6, 2024 hadi Disemba 4, 2024.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara wa TANAPA, Jully Lyimo amewaeleza wanahabari katika mkutano na vyombo vya Habari uliofanyika katika ofisi za TANAPA jijini, Dar es Salaam kuwa lengo la kampeni hii ni kusherehekea miaka 63 ya Uhuru, tukio ambalo ni la kihistoria hufanyika kila mwaka ifikapo Disemba 9.
“Katika sura ya Utalii, TANAPA imekuwa ikitumia fursa hii ya maadhimisho ya siku ya uhuru kuhamasisha watanzania kupanda mlima Kilimanjaro na kutangaza vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kupitia kampeni ya “Twenzetu kileleni”. Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha Watanzania kupanda mlima ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika”.
“Nichukue nafasi hii kuwahamasisha Watanzania wenzangu kushiriki upandaji huu ikiwa ni kuonyesha uzalendo na kupenda vivutio vyetu.
Kwa hivyo kwa mwaka huu ni msimu wa nne wa kampeni hiyo, tunatoa hamasa kwa watu binafsi, watanzania ndani na nje ya nchi, mabalozi, taasisi za Serikali na binafsi kujitoa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi hizi”
"Kama tulivyofanya mwaka jana jumla ya kampuni tatu ndio zimejitokeza kushiriki kampeni hii katika msimu huu wa nne Kampuni hizo ni ZARA Tours, African Zoom na African Scenic,"alisema Kamishna Lyimo.
Kampuni ya ZARA TOURS itatumia njia ya Marangu kama ilivyozoeleka, African Zoom watatumia njia ya Machame na African Scenic watatumia njia ya Lemosho ambapo idadi ya siku za kupanda mlima huo ni 6 kwa njia ya Marangu.
Aidha, siku 7 kwa njia ya Machame na kwa Lemosho itakuwa siku 8 huku Gharama za kupanda mlima zitakuwa ni shillingi 1,550,000/- kwa njia ya Marangu, shillingi
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.