Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwasili Mkoani Arusha siku ya Jumamosi na atapokelewa na uongozi wa Mkoa.
Mhe. Rais akiwa Mkoani Arusha atafanya ziara ya siku 2 katika miradi ya Maji( Jiji la Arusha na Longido), Hospitali ya Jiji na Kiwanda cha Nyama Longido.
Aidha, Mhe. Samia atafanya mikutano ya hadhara 2 katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid na kiwanja cha standi mpya Longido
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amewasisitiza wananchi wote kujitokeza katika mikutano hiyo ya hadhara na barabarani kumlaki.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.