Karibu katika Tovuti ya Mkoa wa Arusha,ambayo inatoa taarifa mbalimbali za Mkoa huu.
Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa Mikoa ya Tanzania na unapatikana upande wa Kaskazini ikipakana na mikoa ya Kilimanjaro na Manyara.Wazawa halisi wa mkoa huu ni wamasai wanaopatikana wilaya ya Monduli,Longido na Ngorongoro ,Wairaki wanapatikana wilaya ya Karatu na Wameru na Arusha.Makabira mengine ni Wasonjo, Wachaga,Wapare,Warangi na Wahadizabe (Tindiga) wanapatikana wilaya ya Karatu hili ni kabila linalotegemea chakula chake kwenye mizizi,matunda,asali na uwindaji,lakini wasonjo wao wamehama kutokana kutegemea chakula cha uwindaji na mizizi mpaka ulimaji wa mazao mbalimbali kama vile mahindi,maharagwe,mihogo na viazi.
Uwepo wa tovuti hii tunatumaini utapata taarifa za kuaminika unazozihitaji kwa ukamilifu kuhusu wigo, upeo wa taasisi, dira, dhamira, malengo, mikakati, shughuli kuu na utekelezaji wa shughuli za Serikali. Katika kufikia dira na matarajio yetu hasa kutangaza shughuli za Serikali lakini pia na huduma zetu kwa umma.
Kupitia tovuti hii tunaamini kwamba itakuwa rahisi kwa wananchi kupata taarifa mbalimbali. Tunatumaini kuwa kila atakayetembelea tovuti hii atapata jambo la kumfurahisha, kumfundisha au kumuelimisha.
Tovuti hii inamilikiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Karibu
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.