Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, amepokea rasmi eneo la bure kutoka kwa kampuni ya Burka Coffee Estate Ltd kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano, hatua ambayo inalenga kuifanya Arusha kuwa kitovu cha mikutano kitaifa na kimataifa.
Katika hafla hiyo, Mhe. Makonda amewapongeza viongozi wa Burka Coffee Estate, kwa kutoa eneo hilo bila malipo, hatua ambayo ni ya kizalendo na inaonesha ushirikiano mkubwa kati ya sekta binafsi na serikali katika maendeleo ya Mkoa wa Arusha.
"Kama tungekuwa tunahitaji kununua eneo hili, tungehitaji fedha nyingi, lakini leo tunalipokea bure — hii ni ishara ya moyo wa upendo kwa taifa letu," amesema Mhe. Makonda kwa furaha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa