Viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, wamemtumia salamu za pongezi na shukurani kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wamemkabidhi Tuzo ya Heshima kwa Mgeni rasmi na kumuomba awafikishie tuzo hiyo kwa kiongozi huyo.
Akiielezea Tuzo hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Ndg. Loy Thomas Ole Sabaya amesema kuwa, hiyo ni ishara ya upendo na shukurani kwa kiongozi huyo mkuu wa Chama, kwa uongozi wake mahiri wenye upendo na kujali wananchi wake, uliowezesha kutekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo kwa kasi kubwa na matokeo yake yanaonekana wazi katika mkoa wa Arusha.
Amesema kuwa, Mkoa wa Arusha umependelewa sana, Mhe. Rais licha ya kutekeleza miradi ya takribani Bilioni 818.63 kisekta kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu, ameweza kusimamia kufufua uchumi wa mkoa wa Arusha, uchumi ambao ulianda kudidimia kwa miaka michache ya nyuma lakini sasa umeinuka kwa kasi, ukiwanufaisha na kuwaneemesha wananchi wa mkoa huo.
Kila mtu ni shuhuda, Kupitia Filamu ya Royal Tour, Hali ya utalii imeimarika, kumekuwa na ongezeko kubwa la watalii, wanaotembelea vivutio vya utalii katika mkoa wa Arusha kwa kuunganisha misimu yote.
mwaka mzima kwa kuzingatia kwamba 80% ya shuguli za utalii nchini zinafanyika Arusha, huku uchumi wa mkoa wa Arusha, ukitegemea.
Hakuishia hapo, mheshimiwa Rais, ameufungua mkoa wa Arusha, uwepo wa Mikutano mikubwa ya kitaifa na kimataifa, umewafanya wakazi wa mkoa wa Arusha kuwa bizy muda wote kupikea wageni, huku wakinufaika kwa kujipatia kipato na kupandisha pato la mkoa pia.
"Nichukue fursa hii, kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Arusha, hususani wanaCCM, tunakuomba utufikishie salamu zetu za shukani kwa Mheshimiwa Rais wetu, mwambie Arusha tuko salama, tuko nyuma yake, hatutamuangusha, tunapiga kazi, huku Kazi Inaendelea" Amebainisha Mwenyekiti Ole Sabaya.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa