KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema Maonyesho ya Kimataifa Utalii ya ‘Karibu KiliFair’ ni mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine ya kitalii ili kuchangia kukuza utalii.
Pia amesema Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda anamuwakilisha vyema Rais Samia Suluhu Hassan kwani ametaka utalii ukue na amekuwa akifanya juhudi za kukuza utalii kwenye mkoa huo, kuchochea suala la utulivu na amana na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.
Makalla ameeleza hayo leo Juni 6,2025 wakati alipotembelea maonyesho hayo yaliyoandaliwa katika eneo la viwanja vya Magereza mkoani Arusha akiwa njiani kuelekea Arusha mjini kwa ajili ya mkutanona hadhara akiendelea na ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa