Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Meru na Afisa mwandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga Kura Jimbo la Arumeru Mashariki, Mwl. Zainabu Makwinya amefungua Mafunzo kwa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata, Desemba 04,2024.
Mwl. Zainabu, amewasisitiza maafisa hao kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa kuwa ndio msingi na maelekezo ya zoezi zima wanalokwenda kulifanya la Uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni maandalizi Bora ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani 2025.
Aidha Mwl. Makwinya amewataka wasimamizi hao kuongeza umakini kwenye mambo ambayo ni mapya kwa kuzingatia teknolojia inayotumika ni mpya hivyo waache kuchukulia mambo kwa urahisi na kusema kuwa walishakwisha kufanya kipindi cha nyuma na badala yake kuwa makini na kuingiza kitu kipya ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wa Zoezi liloko mbele yao.
Hata hivyo, Waandikishaji hao wamekula kiapo cha usiri na kiapo cha kujiengua kwenye vyama vyao vya Siasa ili kuwapa fursa ya kufanya kazi hiyo kwa uhuru na haki.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa