Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amewasili Mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda pamoja na viongozi wengine wa Chama cha Mapinduzi na Serikali, leo Juni 04, 2025.
Makamu wa Rais amefika mkoani Arusha kwaajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa 55 na Kongamano la Kisayansi la mwaka la Chama cha Wafamasia Tanzania linalofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mikutano (AICC) Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa