Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Mrisho Gambo amesema bado mkoa unaitaji kujipanga zaidi katika swala nzima la lishe na kuongeza nguvu zaidi katika kutoa elimu katika jamii ili dhana hii iweze kueleweka.
Amewataka wataalamu wa lishe kujipanga zaidi ili kuhakikisha fedha zinatengwa kama ilivyopangwa na elimu inapelekwa kwa wananchi, ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha pili cha tathimini ya hali ya lishe cha mkoa kwa mwaka 2019/2020.
“Inashanganza sana kuona baadhi ya halmashauri zinashindwa kutoa fedha kiasi cha shilingi 1000 kwa kila mtoto wakati kwenye bajeti zenu mliziweka,sijui shida iko wapi?’’.
Nae mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dr. Wedson Sichalwe amesema, mkoa umeweka juhudi katika kushirikisha wadau mbalimbali kama vile viongozi wa dini, viongozi wa kimila na taasisi binafsi ili kuhakikisha elimu ya lishe inafika mbali zaidi.
Amesema kama viongozi wa dini wao wana waumini wakutosha wakizungumzia maswala haya ya lishe itarahisisha zaidi elimu kuwafikia wengi na viongozi wa kimila hali kadhalika wanajua namna yakutoa elimu hiyo kwa jamii zao wakizingatia mila na desturi za sehemu husika.
Sichalwe amesema pia wadau wa moja moja ambao mkoa unafanya nao kazi pia wanamsaada mkubwa wa kuhakikisha elimu ya lishe na ufanikishaji wa afua zake zinawafikia wananchi kwa urahisi.
Mzee wa kimila hali maarufu kama Laigwanani ,Tobiko Kivuike na Isack Lemsongo wameiyomba serikali kuongeza juhudi zaidi ya utoaji wa elimu ya lishe,iCHF na afya ya uzazi na mtoto katika jamii za kimasai zaidi kwani wengi wao hawana ufahamu nayo.
Wamesema sababu kubwa katika jamii hizo ni mila na desturi za Kimasai zinawafanya wananchi wengi kutotilia mkazo au kuona umuhimu wa haya mambo.
“Ni vema wataalumu wa afya wakaongezwa katika zahanati za kijiji na wakaajiriwa wataalamu maalumu wakutoa elimu hii ya lishe kuliko kusubiri watalaamu wa mjini wanaokuja mara moja moja”,alisema Tobiko.
Pia walipendekeza katika utoaji wa elimu ya afya ya uzazi na mtoto wanandoa wote wahusishwe kwani katika jamii za kimasai wanaume wengi hupinga sana maswala ya uzazi wa mpango na hivyo kuwa kikwazo kwa wake zao ambao wanataka kutumia njia hizo.
Kikao cha lishe cha mkoa hufanyika kila baada ya robo mwaka wa fedha ili kutadhimini hali ya lishe katika mkoa na changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hiyo katika kufikisha malengo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa