Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa,amefurahishwa na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Karatu ambao upo katika hatua za mwisho kukamilika.
Ameyasema hayo, alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ijayo.
Amesema, kukamilika kwa Hospitali hiyo kutaleta unafuu kwa wananchi wa maeneo ya jirani kwani wataweza kupata huduma za Afya za uhakika na karibu.
Ujenzi wa Hospitali hiyo umegharimu bilioni 2.9 ambapo Serikali imetoka bilioni 1.7 na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wametoa Milioni 700.
Hadi Sasa tayari majengo ya wodi ya wazazi,mionzi, kufulia, dawa, huduma za dharura, nyumba ya watumishi, jengo la wagojwa wa nje na maabara yapo katika hatua za umaliziaji na huduma itaanza kutolewa mapema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dadi Kolimba amesema wameweka nguvu kubwa katika Hospitali hiyo kwani Wilaya hiyo haijawai kuwa na hospitali ya Wilaya.
Amesema wanaendelea kuhakikisha Hospitali hiyo inaanza kazi mapema iwezekanayo kwani ujenzi uliobaki ni kidogo sana.
Katibu Tawala amefanya ziara ya siku moja Wilaya ya Karatu na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo Shule, kituo cha Afya na hospitali ya Wilaya kwa lengo kujiridhisha na kazi zinavyofanyika.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa