• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

JESHI LA POLISI LAPONGEZWA KUIMARISHA USALAMA MKOA WA ARUSHA

Posted on: January 26th, 2024


Na Elinipa Lupembe


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amelipongeza Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, kwa kufanya kazi kwa weledi na kushirikisha jamii, jambo ambalo linazidi kuimarisha usalama wa mkoa wa Arusha, mkoa ambao shughuli ni kitovu cha Utalii nchini.


Mhe. Mongella ametoa pongezi hizo wakati wa sherehe za kuwapongeza Askari wa Jeshi la Polisi waliofanya kazi vizuri na waliostaafu utumushi wa Umma,  mwaka 2023, zikiwa ni sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2024, zilizoandaliwa na Jeshi hilo mko wa Arusha na kufanyika kwenye hoteli ya Primier eneo la Sakina Wilaya ya Arumeru.


Amethibitisha kuwa, hali ya utulivu na amani ya mkoa wa Arusha, ni matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi kupitia dhana ya ulinzi shirikishi kati ya Jamii na Jeshi hilo, unaopelekea jamii kushiriki katika ulinzi na usalama inasababisha utulivu wa hali ya juu na kuifanya jamii kujikita lwenye shughuli za uzalishaji kwa maendeleo ya jamii na taifa.


"Serikali kupitia dhana ya ushirikishwaji wa jamii katika ulinzi na usalama, inaunganisha moja kwamoja na mchakato wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, amani ya mkoa wa Arusha inasababisha wananchi kufanya kazi na sio kupambana na migogoro isiyo ya lazima" Amsema Mhe. Mongella.


Ameongeza kuwa, Matunda ya Utalii mkoani Arusha yaliyochochewa na tamthilia ya Royal Tour iliyofanywa na Me. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yanachachushwa na Jeshi la Polisi kwa kuimarisha Ulinzi na Usalama kuhakikishia ulinzi wa watu na mali zao


Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi, ACP Justine Maseja, amesema kuwa ni desturi ya Jeshi hilo la Polisi, kukutana pamoja nje ya kazi walau mara moja kwa mwaka ili kuopongezana Askari Polisi, waliofanya vizuri kwa mwaka husika, kuwapongeza Askari

waliolitumikia Jeshi hilo na hatimaye Kustaafu kwa mujibu wa sheria pamoja na  kubadilishana mawazo nje ya eneo la kazi.


"Kwa mwaka 2023 tunawapongewa Askari 30 waliofanya kazi vizuri na askari 39 walolitumikia Jeshi la Polisi na kustaafu kwa mujibu wa sheria mwaka 2023, tunatoa vyeti vya pongezi ikiwa ni ishara ya kuthamini kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kulitumikia Taifa kupitia Jeshi letu la Polisi" Ameweka wazi RPC.


Hata hivyo, Mwenyekiti wa TATO Henry Kimambo, amesema kuwa, Sekta ya Utalii ina uhusiano mkubwa na Jeshi la Polisi, kutokana na ukweli kwamba, hulka ya watalii ni kutembelea maeneo ambayo kuna hali ya amani na  utulivu


"Kabla mtalii hajafanya maamuzi ya kutembelea vivutio vya utalii, hutazama kwanza hali ya amani na utulivu wa nchi husika, mambo mengine hufuata baada ya kujihakikishia usalama, nchi yetu imeweka mipango imara kwa kuwa na ushirikiano kati ya sekta ya Utalii na Jeshi la Polisi" Amesema Kimambo


#arushafursalukuki 




                        
                       
                        </div>
                        <!-- /.right-sidebar-content -->
                        <!--/END RIGHT SIDEBAR CONTENTE SECTION-->
                    </div>



<div class=

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa