Halmashauri ya Jiji la Arusha, wametekeleza agizo la Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, aliyeagiza kukarabati vyumba vya vinne vya madarasa shule ya sekondari Terrat.
Baada ya maelekezo hayo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Mhandisi. Jumaa Hamsini, amesema kuwa tayari wametekeleza agizo la RC, kwa kukarabari vyumba vinne vya madarasa na kuweka madawati, madarasa ambayo wanafunzi wa kidato cha kwanza wanasoma kwenye madarasa hayo.
Amesema kuwa, ukarabati huo umetumia kiasi cha shilingi milioni 20, fedha za mapato ya ndani, ukarabati ambao ni muhimu kutokana na idadi ya wanafunzi waliopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza shuleni hapo mwaka 2024.
Jumla ya wanafunzi 550 wamepangiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo ulioanza 08 Januari, 2024 shule ya sekondari Terati, huku wanafunzi 485 wakiwa tayari wameripoti na kuanza masomo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa