Kufuatia Kiliniki ya matibabu yaliyotolewa bure kwenye kambi ya madaktari Bingwa na mabingwa Wabobezi iliyofanyika kwa siku 7 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha, jumla ya wagonjwa 32, 136 wastani wa wagonjwa 4,598 kwa siku, wamepatiwa huduma za matibabu, vipimo, dawa na vifaa tiba.
Taarifa hiyo imetolewa na Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Charle Mkombachepa, kwa waandishi wa habari wakati wa kufunga rasmi Kambi hiyo Julai 01, 2024 ikiwa ni siku ya nane kati ya siku 7 zilizopangwa kukamilisha kambi hiyo.
Dkt. Mkombachepa amesema kuwa kambi hiyo ilianza tarehe Juni 24 ikiwa na wahudumu wa afya 450, ikiwa na lengo la kuhudumia wagonjwa 7,000 kwa wastani wa wagonjwa 1,000 kwa siku, lakini kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi waliofika kupata huduma kwenyw kambi hiyo ililazimika kuongea watoa huduma na kufikia 550, walioweza kufanikisha kuhudumia wagonjwa hao 32, 136.
Aidha ameainisha wagonjwa hao, 32,136, jumla ya wanawake 19,546 sawa na 60.7, wanaume 12,640 sawa na 39.3 na watoto 4,616 sawana 14.3, waliweza kupata huduma za matibabu na vipimo ambavyo wananchi wenye kipato cha chini wasingeweza kumudu gharama za vipimo hivyo.
Amefafanua kuwa, pamoja na huduma zilizotolewa za vipimo wagonjwa 20 walipimwa kipimo cha RMI, wagonjwa 180 walifanyiwa kipimo cha CT - Scan, wagonjwa 1,820 walipewa rufaa kwenda hospitali ya Mount Meru ambapo 14 tayari wamefanyiwa pasuaji huku wagonjwa 31 wakiwa kwenye ratiba ya upasuaji, na kuongeza kuwa wagonjwa 170 wamepewa rufaa ya kwenda hospitali nyingine za rufaa wagonjwa 265 JCKI, wagonjwa 69 MOI, wagonjwa 20 Hospitali ya Taifa Muhimbili, wagonjwa 2 Benjamin Mkapa na wagonjwa 2 hospitali ya Mirembe za Dodoma.
Hata hivyo, Dkt. Mkombachepa amempongeza na kumsukuru mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye, kambi hiyo ilikuwa ni maono yake yakiwa na lengo la kutoa hudma za afya bure kwa wananchi wasio na uwezo wa kuoata huduma hizo kutokana na kipato duni na hatimaye utekelezaji wake umezaa matunda mema yaliyorejesha matumaini kwa wagonjwa wengi.
Zaidi amewashukuru wadau wote waliojitoa kwa hali ja mali kukamilisha zoezi hilo muhimu wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuunga mkono kambi hiyo kwa kutoa dawa na vifaa tiba pamoja na kupiga simu ya kuwatia moyo watoa hudumu pamoja na kuwapa pole na kuwafariji wagonjo wote.
Awali, ametoa wito kwa wakazi wa Arusha kuwa, wagonjwa wengi wameonekana kuwa na magonjwa yasiyoambukiza, magonjwa ambayo yanaweza kuepukika kwa kuzingatia taratibu za kiafya ikiwemo kufanya mazoezi, lishe bora, usafi binafsi na usafi wa mazingira, kuepuka ulevi wa kupindukia, uvutaji wa sigara, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa