Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), wamepongeza hali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Longido Sekondari - Kanisa la KKKT iliyojengwa kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa mita 500, kipande ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 500 fedha za Mfuko wa Jimbo.
Wajumbe hao, wamepongeza hali ya ubora wa barabara na kiwango cha lami kichojengwa kwenye barabara hiyo yenye mitaro ya kupitishia maji pamoja na vivuko vya kisasa, vinavyoendana na kiwango cha barabara hiyo, wakati walipotembelea na kukagua maendeleo ya utekelzaji wa mradi huo.
Licha ya kuridhishwa na ubora wa mradi huo, wamewapongeza wasimamizi na Mkandarasi wa mradi huo, na kuzitaka halmashauri nyingine kuiga mfano huo, huku wakisisitiza Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha, Mameneja wa TARURA wanasimamia fedha katika hatua zote za utekelezaji wa miradi ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha inayotolewa na Serikali.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Justine Nyamoga, amewapongeza viongozi, watalamu na wananchi wa Longido kwa ushirikiano wao katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuwata kuendelea kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ikiwa ni pamoja na kutoa fedha nyingi za miradi ambayo inatoa huduma kwa wananchi ikiwemo afya, elimu na barabara.
Hata hivyo ameitaka TAMISEMI kupitia Wakala wa Barabara mijini na vijijini (TARURA), kuwaangalia wakandarasi wenye uwezo wa kufanya kazi kwa wakati na yenye viwango vya ubora, kuhakikisha wanawalipa fedha zao kwa wakati pindi wanapokamilisha taratibu zote za kazi.
"Waangalieni wakandarasi kama huyu, aliyejenga barabara hii, barabara ni nziri imejenhwa kwa viwango vya ubora pamoja na kukamilisha kwa wakati licha ya changamoto zilizopo, walipwe fedha zao ili kuwatia moto wasikate tamaa ya kufanya kazi za Serikali." Amesema Mhe. Nyamoga.
Naye mjumbe wa Kamati Mhe. Hawa Mwaifunga (Mb), ameshangazwa na ubora wa barabara hiyo, ubota ambao ni tofauti na maeneo mengine waliyopitia licha ya kuwa kiwango cha fedha kilichotolewa kinaendana na kusisitiza kufanya tathmini pindi fedha zinazotolewa ziweze kutekeleza miradi kwa viwango vya ubora unaendena kwenye maeneo yote.
Akiwasilisha Taarifa ya mradi huo, Meneja wa TARURA mkoa wa Arusha Mhandisi. Laynas Sanya, ameweka wazi kuwa, lengo mradi huo, licha ya kurahisisha hali ya usafiri kwa wananchi zaidi una lenga kupandisha hadhi barabara za wilaya ya Longido.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa