Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb) leo tarehe 29 Oktoba, 2023 amemuapisha Richard Rwanyakaato Kiiza kuwa kamishna wa Uhifadhi wa mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) baada ya Uteuzi uliofanywa na mhe. Rais hivi karibuni.
Katika tukio hilo Mhe. Waziri amebainisha kuwa Uteuzi wa Kamishna huyo ni sehemu ya kuimarisha majukumu ya Uhifadhi, utalii na maendeleo ya Jamii na kuongeza kasi ya kutangaza utalii kwa njia mbalimbali za kisasa ili kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea nchi yetu kama ilivyo adhima ya Mheshiwa Rais wetu.
Waziri Kairuki ameilekeza bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kusimamia sheria za uhifadhi ikiwemo kutoa mifugo yote iliyoingiza kinyemela katika maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo Pori tengefu la Loliondo.
“Pamoja na majukumu mengine mliyonayo nawaelekeza wahifadhi kusimamia sheria zilizopo na kuhakikisha mifugo iliyoangizwa kinyemelea katika maeneo ya Hifadhi iondolewe” amesisitiza mhe. Kairuki
Aidha Mhe. Kairuki amempongeza Kamishna wa Uhifadhi aliyemaliza muda wake, Dkt. Freddy Manongi kwa juhudi ambazo wamezifanya katika kutangaza Vivutio vya utalii tulivyonavyo ambapo juhudi hizo zimeiwezesha Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) kuchaguliwa na mtandao wa “Word Travel Awards” kama kivutio bora cha Utalii barani Afrika “Africa Leading tourist Attractions” na mafanikio ya kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia wageni zaidi ya 752,000, kuongeza mapato hadi kufikia Bilioni 171 mwaka wa fedha 2022/2023
Vilevile Mhe. Kairuki amemuelekeza Kamishna wa Uhifadhi NCAA na wadau wengine wanaohusika na zoezi la zoezi la uelimishaji, uandikishaji, uthaminishaji na uhamishaji wa wananchi wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wanaojiandikisha kuhama kwa hiari kuendelea kusimamia eneo hilo kwa kufuata sheria na misingi ya haki za binadamu.
“Serikali inaendelea kuwahakikishia Wadau mbalimbali, Wananchi wa Ngorongoro na Jumuiya za Kimataifa kuwa zoezi hili ni la hiari, shirikishi na linazingatia misingi ya haki za kibinadamu na utawala bora na kila mwananchi aliejiandikisha kuhama kwa hiari Serikali itampa fidia na gharama zote za kumhamisha hadi alipochagua kwenda zinabebwa na Serikali kwa asilimia 100” amesisitiza
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa